Tuesday, March 5, 2013

BREAKING NEWS: MOTO MKUBWA WAZUKA DAR LEO

Moto mkubwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo kama uonekanavyo pichani.
Moto mkubwa umezuka na kuteketeza mali mbalimbali zilizokuwemo kwenye moja ya ghala kubwa la kuhifadhia vitu mbalimbali ikiwemo vikombe vya udongo,Pampas,vigae na vitu vingine,sehemu ya maghala ya kuhifadhia vitu Shekilango,jijini Dar,aidha kufuatia tukio hilo mpaka Globu ya Jamii inaondoka eneo la tukio,hasala naa gharama za mali zilizoteketea haikuweza kufahamika mara moja,aidha kwa mujibu wa Kamanda wa mkoa wa Kipolisi Wilaya ya Kinondoni,Afande Kenyela alieleza kuwa mpaka sasa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika isipokuwa juhudi za kuuzima moto zilikuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Ultimate Security wakiendelea kuzima moto uliokuwa ukiendelea kuwaka ndani ya ghala hilo,ambao tayari ulikwisha teketeza mali nyingi.
No comments: