Balozi wetu Marekani Mama Mwanaidi Maajar-Sinare akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Rais wa kampuni ya Asian Global Management,LLC,Dr Jes Tarp akizungumza na wanahabari katika uwanja wa KIA ,Muda mchache baada ya kuwasili nchini kwa ajili ya V.I.P Safari iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Balozi Majaar na wageni wake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya Safari ya Marais,Wenyeviti,Wakurugenzi wa makampuni mbalimbali ya nchini Marekani ambao wamekuja Tanzania kwa ajili ya kutengeneza diplomasia katika masuala ya uchumi.
PICHA NA HABARI NA MWAKILISHI WETU TOKA BONGO
Akizungumzia ugeni huo balozi Maajar amesema wakuu hao wa kampuni mbalimbali zaidi ya 17 wamekuja nchini kuangalia maeneo ambayo wataweza kuwekeza hususani katika sekta ya nishati,Kilimo,Usafirishaji na utalii.Amesema ujio huo umeandaliwa na ofisi yake ukijulikana kama V.I.P SAFARI ambapo leo mchana watakula chakula cha pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa mjini Arusha yaani Business Lunch na baadaye watakutana na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Isdor Shirima kwa ajili ya chakula cha jioni.Amesema wakiwa nchini wageni hao watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii kabla ya kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maonesho ya Saba saba na baadaye kula chakula cha pamoja na rais Jakaya Kikwete.Balozi Maajar amesema pia wageni hao watatembelea Zanzibar ambapo watakuwa wageni wa rais wa Zanzibar Dk Ally Mohamed Shein ambapo pia watapata fulsa ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya
utalii katika mji wa Zanzibar.
No comments:
Post a Comment